HISTORIA YA JACK CHAIN.
MCHEZAJI MAHIRI WA MICHEZO YA KARATE ,NA STLYE ZINGINE ZA MAPIGANO,NA MWENYE VIPAJI VINGI PAMOJA NA UIGIZAJI,ACROBATIC,NA HATA UIMBAJI.
Jack chain kazaliwa 7 April 1954 katika eneo liliofahamika kama British Hong Kong kipindi cha ukoloni . Jina lake halisi ni Chan Kong Sang , Bali jack ni jina la usanii tu ama jina katika fani yake ya uigizaji.
 |
| JACK KWENYE POSE KALI LA MAPIGANO. |
Baba yake ni Charles chan na Mama Lee Lee Chain refugee from the Chinese Civil War. kabla ya kubadili kazi bwana Charles chan .Jack akiwa mdogo alibatizwa jina la utani kama pao pao yaani kitenesi (cannonball) kutokana na wepesi wake wa kuruka ruka .
 |
| JACK CHAIN IKIMPA MAFUNZO JADEN SMITH MTOTO WA WILL SMITH KWENYE KARATE KIDS |
 |
| JACK AKIMNOA JADEN SMITH KWENYE KARATE KIDS |
Jack alianza masomo yake ya awali, katika shule ya msingi ya Nah- Nhwa kisiwani HongKong Hata hivyo alifeli kwa mwaka wake wa kwanza. wakati huo Wazazi wake walikuwa wafanya kazi katika balozi ya Ufaransa ndani ya jiji la Hong Kong .na Jack alikulia pembezoni mwa wilaya ya Victoria Peak consul’s redendence ndani mji huo wa Hong Kong.
Ila hatimae mwaka (1960)wazazi walihama na kelekea katika mji Canberra inchini Australia,ambapo baba yake alikwenda kufanya kazi, kama mpishi mkuu katika balozi ya Marekani,Hivyo Jack alipelekwa nchini China kusoma katika chuo cha sanaa ya maigizo na michezo.A Perking Opera School .(Drama Acamemy)
chini ya Master Yu Jim –yuen. Jack alichukua mafunzo kwa miaka 10. katika martial arts na Acrobatics (sarakasi na mapigano).
 |
| KUTOKA KUSHOTO YUEN BIAO KATI SAMO HUNG NA KULIA JACK CHAIN |
Na hapo ndio alipopata nafasi ya kuingia katika Seven little Fortune (saba wenye bahati) jina lake la kisanii alifamika kama Yuen Lo kwa wakati huo, ambalo hilo lilikuwa ni jina la master wake.aliungana na marafiki wawili vipenzi amabyo baadaye walikuja kujulikana kama (Three brothers ama three Dragons, Sammo Hung na Yuen Biao.)
 |
| kutoka kushoto ni Jack kati ni Samo hung na kulia ni Yuen Biao |
NI NANI ALIMBATIZA JINA LA (JACK)
Mwaka 1976 Jack alirudi Australia kwa wazazi wake na kujiunga chuo cha Dickson ama (Dickson College) na kufanya kazi za ujenzi (Mmoja wa mafundi (costruction worker) aliyetambulika kwa jina moja la Jack,Ndie aliyembatiza jina hilo la utani.kwani alishindwa kutamka jina lake halisi kwa kichina yaani Chan Kong Sang.hatimaye akajikuta kapewa jina jack badala yake.au a little Jack (jack mdogo) ama Jackie,aliendelea kulitumia jina hilo kwa kipindi kirefu ,mpaka alipokuja kulibadili mwishoni mwa 1990 na kuitwa jina lake la ukoo (Fong Si –Lung).Ambalo ndilo likuwa jina upande wa ukoo wa baba yake.
NI WAPI ALICHUKUA MAFUNZO ZAIDI YA MAPIGANO.
 |
| JACK KATIKA POSE LA SNAKE |
Baada ya kuingia katika industry filamu Jack na sammo Hung waliapata nafasi ya kuchukua mafunzo ya Hapkido chini ya master Jin Pal Kim. hatimaye Jack akapata mkanda mweusi (black belt).
Aliendelea kujifunza style zingine za mapigano zaidi za Martial arts kama vile Karate,judo,taekondo na Jeet Kune Do.
Baada ya kuingia katika industry filamu Jack na sammo Hung waliapata nafasi ya kuchukua mafunzo ya Hapkido chini ya master Jin Pal Kim. hatimaye Jack akapata mkanda mweusi (black belt).
Aliendelea kujifunza style zingine za mapigano zaidi za Martial arts kama vile Karate,judo,taekondo na Jeet Kune Do.
 |
| JACK CHAIN AKICHUKUA MAFUNZO |
LINI ALIANZA KUGIZA?
Alianza kuigiza tangu akiwa mdogo na kutokea katika scene chache tangu akiwa na umri wa miaka 5 .Ila alipofikisha umri wa miaka8 alionekana kwenye little Fortune katika filamu ya Big an Little Wong Tin Bar (1962)akiigiza na mwanadada Li li Hua kama mama yake,Na hata hivyo alitokea tena na mwanadada katika filamu The Love Eterne (1963)Pamoja na part mbalimbali za filamu ,katika KING HU’S mwaka 1966 ya Come drink with me. Baada ya kutokea katika filamu kadha za Kung fu ikiwemo ya A touch of Zen,ndipo aliposaini na Chu Mu;s Great Earth Film Company ,akiwa na umri wa miaka 17.Na kuanza kufanya kazi kama Stuntman (michezo ya Hatari) kwenye filamu aliyocheza na Bruce lee ya Fist of Furry na Enter the Dragon akitumia jina la kisani kama Chan Yuen Lung.
Hapo Ndipo alipopata nafasi kwa mara kwanza kuigiza kama muigizaji nyota ( movie star)katika filamu ya Little Tiger of Canton ambapo ilizuiwa kutolewa 1973 na hatimaye ikaruhusiwa mwaka 1978 .ilikuwa ni filamu kali,ambapo jack alicheza kama kijana alikuja kulipiza kisasi juu ya kifo cha baba yake akitokea kwenye kundi la siri la uharifu huko inchini china.
Kutokana upungufu wa fedha za kuwekeza katika filamu na michezo ya stunt 1975 kuyumba. Jack aliamua kuingia kwenye filamu za Comedic pamoja na Adult film,Ikiwemo All in the Family,na hii ndio ilikuwa filamu yake ya kwanza kuigiza utupu na pia filamu yake ya kwanza kuigiza bila ya scene ya mapigano wala michezo ya stunt. Na hata hivyo Jack akatokea tena katika sex scene ya Shinjuku Incident
JACK CHAIN NA MUZIKI AKIPERFOM
 |
| JACK CHAIN AKIIMBA |
Mbali na uigizaji jack ni mwanamuziki, Na keshatoa records mbalimbali,Akiwa mdogo alikuwa akihudhuria Mafunzo ya kuimba, The Peking Opera school.Alianza kuimba toka mwaka 1980, na kumfanya kuwa ni mwanmuziki mwenye mafanikio makubwa huko Hong na Asia.
Amekwisha toa Album takrbani 20 toka mwaka 1984.Amekuwa akiimba katika lugha tofauti KIJAPANI,Mandarini, Cantonees ,Kitaiwaini na Kingeleza.
Karibu filamu zake zote Sauti za nyimbo zinazosikika mwisho wakati picha inaisha ni nyimbo alizoimba Jack chain.
Wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni ‘’kung Fu fighting man”wimbo huu utausikia katika filamu ya The Young Master (1980) mwishoni wakati maandishi yapanda kuonyesha washiriki wa filamu.Karibu ya record zake 10 zimekuwa zikitumika kama soundtrack album za filamu zake.
Wimbo wake aliouimba katika lugha ya Cantones story of hero unaweza kuusikia katika filamu ya police story, na ulichaguliwa na Royal Hong Kong Police na kuuingiza katika Idara yao ya Matangazo 1984. HEBU FUATILIA UJUE MENGI USIOYAJUA KUHUSU JACK NA FAMILIA YAKE .inaendeleaa........
 |
JACK CHAIN KUSHOTO NA MWANAYE WA KWANZA KULIA JAYCEE CHAIN
|