
Somo letu kubwa lipo kwa ndege anayepatikana
huko
Sourethern hemisphere,pembezoni mwa Antarctica,Pia wanapatikana South America,
south Africa,New Zealand na maeneo mengi ya visiwa vya Pacifici .
kuna mambo makuu mawili ya kujifunza yanayofanana juu ya ndege huyu,hasa kwa wazazi na wanajamii wengine ambao pia wanataraji kuwa wazazi hapo baadaye.kama ilivyo kwa manadamu kuna mgawanyo wa majukumu kati ya baba na mama ndivyo ilivyo kwa ndege huyu.
![]() |
![]() |
| PENGUINE AKILISOGEZA YAI LAKE TAYARI KULALIA |
Sasa ukiwa kama baba unatakiwa kutimiza jukumu lako la kuitunza na kuilinda familia kuhakikisha wanakula kuvaa na kadhalika na si kukimbia familia.kwani unadhani ambaye anapaswa kuingalia familia yako kama si wewe ni nani,tazama mfano wa ndege huyu namna anavyopitia shida mbali mbalimbali lakini bado hulitunza yai lake ama kifaranga matarajiwa asidhurike na majanga kadhaa.Usikimbie majukumu wajibika ,kuwa mwanamme sahihi kwa kutimiza majukumu yako,Vipi ungependa kuitwa mwanaume Suruali BASI WAJIBIKA.No way out.
![]() |
JAMBO LA PILI LA KUJIFUNZA NI KUWA.
Inapotokea Penguine kapoteza mtoto ,basi huweza kuipa mtoto kutoka familia nyingine ya pengiune,ili mradi achukue nafasi ya mtoto aliyepoteza haijalishi si wa kwake.
Tazama ni njinsi gani ndege HUYU alivyo na Ufahamu mkubwa na kujua thamani ya familia ,yuko radhi aibe mtoto toka jamii nyingine,ili mradi apate faraja kwa kifarnga aliyepotea

SASA TUGEUKE KWA MWANADAMU
Hebu tazama kwa wale ndugu zetu ,haijalishi
mwanamke au mwanaume ,dada au kaka mnaotupa watoto au kuwatelekeza watoto.Hivi unafikiri ni nani mwenye akili wewe uliepita nakuvuka madarasa toka ,Nursery,secondary hadi chuo kikuu na mwenye elimu kubwa,ama huyu ndege asiyejua kusoma wala kuandika na asiyejua nini maana ya utandawazi, facebook ,whatsup na Instragramu.Bila kujali chakula atakipata wapi bado atahakikisha anatimiza majukumu yake ni pamoja na kumlinda mwanaye na kumuweka mahali palipo salama na si kumkimbia.
![]() |
| Penguine akifunika mwanaye dhidi ya Baridi |
Ikiwa MUNGU aliyekuumba kasema wewe mwanadamu,ni mwenye akili kuliko viumbe wote na wako chini yako,iweje kiumbe huyu akushinde.TAFAKARI CHUKUA HATUA USIKIMBIE MAJUKUMU.
TIMIZA WAJIBU WAKO.



