Ijumaa, 18 Novemba 2016

SOMA HISTORIA ZA MASTAA TOKA MAREKANI KABLA YA KUWA MASTAA,FAMILIA ZAO,NA SASA NI MASTAA.HUWEZI AMINI WALIKOTOKA.

             


                              

                        UNDERTAKER 


   
   Kama wewe utakuwa ni
 mfuatiliaji mzuri wa mieleka ,Jina Undertaker Halitakuwa geni masikioni mwako,kwani mmoja kati ya wachezaji tishio katika  industry ya Mieleka ,(wrestling)


Undetaker anavyokuja
Kutokana na ujio wake Ulingoni mara Taa huzimika ghafla, zinapowashwa mara mtu yuko ndani ya Ulingo simchezo,sifa yake kubwa Huwa si muongeaji bali ni mtu wa Vitendo,amekuwa akifanya vizuri karibu Mapambano yake yote.


Mara Undertaker Ulingoni  

Undertaker ni nani basi.(Ni mchezaji Mieleka wa kimarekani)na hilo ni  jina lake bandia la(ulingoni)

Undertaker kono la Chuma

   Undertaker jina lake halisi ni Mark Wiliam Calaway.kazaliwa 24 march 1965 Houston ,Texas Inchini Marekani.
Wazazi wake Baba ni bwana Frank Compton Calaway,na mama ni Betty Truby Catherine.


   Elimu yake ya secondary kaipatia katika shule  ya secondary Waltrip High school ambapo huko alikuwa member katika timu ya mpira wa rugby(america football)na Basketball.
Undertaker akicheza Basketball akiwa high school mwenye namba 33 kifuani kushoto.
Ila alifanikiwa kugraduate 1983 na kisha kujiunga na chuo cha Angelina college,katika mji wa Lufkin texas on basketball scholarship.
  Mwaka 1985 alisajiriwa kwenye chuo cha Texas Wesleyan University ndani ya mji wa Fort Worth miongoni mwa miji mikubwa katika jimbo la Texas akichezea timu ya basketball,alikuwa mtu muhimu kwenye sport management, Alicheza  nafasi ya kati kama mtu mwenye nguvu ,mrefu na mwenye uzito kamili Big man ni mtu muhimu mwenye sifa kati ya moja ya nafasi tano muhimu kwenye mchezo wa basketball toka mwaka 1985 mpaka 1986.


Undertaker in Basketball team.

  Ila ilipofika mwaka 1986 Undertaker aliachana na chuo na kujikita zaidi kwenye michezo ,Ukweli alipenda  sana kuwa profession basketball(mchezaji basketball) huko uraya ,kabla hajamua na kubadili fikra zake  na kujikita katika mchezo wa mieleka(professional  wrestling) mwalimu wake wa mieleka alikuwa ni Don Jardine.

KATIKA MICHEZO YA MIELEKA


Undertaker kulia na Cane kushoto..
  Undertaker aliingia kwa mara ya kwanza ulingoni kwenye (WCCW)World Class Championship Wrestling)akitumia jina la  Texas Red, ila alipoteza mechi hiyo alipopambana na Bruiser Brody.hatimaye mwaka 1988 baada ya miaka minne ya Promotion,Alitoka huko na kujiunga na Coninental Wrestling Association,ambapo alikuja kuwa sehemu ya United Wrestling.
UNDERTAKER ALIYESIMAMA KWENYE HELL IN THE CAGE
UNDERTAKER ALIYESIMAMA NA KAVAA GLOVES
HIVI NDIVYO ANAVYOMALIZAGA GAME UNDERTAKER


MCHEZO HUU NI HATARI USIIGE WALA KUJARIBU
HUYU UNDERTAKER NI BALAA.
Association hiyo ni baada ya Jerry Jarrett Kuinunua WCCW na kuzuka taasisi mbili ndani ya taasisi moja



Billionea Dolnad Trump Rais wa Marekani kwa sasa kwenye Mieleka wakimnyoa Jamaa Nywere kwa nguvu akiwa kashikwa na mabaunza.wakwanza toka kushoto aliyeshika mashine na Tai Nyekundu.Kabla ya Hajawa Rais.
  • USHABIKI NA MARAFIKI VIPENZI
  •   Ingawaje ni mchezaji mzuri wa mieleka hata hivyo pia ni mshabiki mkubwa wa, boxer .


  • UNDERTAKER  Jamaa alivaa kiremba AKIHOJIWA KWENYE PAMBANO KATI YA PACQUAIO VS VELAZQUEZ
    Kulia Pacqiuao na Valazquez kushoto

    kuna wakati aliwahi,kuonekana akiwa kabeba bendera ya Marekani akiongozana na mashabiki wa Pacquiao 
    PACQIUAO MWENYE KAPTULA NYEKUNDU  NA VALAZQUEZ ALIYEPIGA MAGOTI CHINI,


    wakielekea ulingoni kwenye mechi kati ya Pacquiao na Velazquez mwaka 2005.Na pia alionekana akifuatilia kwenye pambano kati ya Lennox Lewis na Mike Tyson mwaka 2002.
    MIKE TYSON KULIA NA  LENOX LEWIS KUSHOTO  
    rafiki zake wa karibu ni pamoja  Mwigizaji Tony Longo ,na amendelea kuwa karibu na marafiki hao wachezaji wa mixed martial artist
    TONY LONG UNDERTAKER FRIEND


    (wachezaji wenye kuchanganya karate na mapigo mengine) Pat Miletich,Jeremy Horn na Matt Hughes.
WATOTO NA WAKE ZA UNDERTAKER
Undetaker keshaoa  mara tatu na kuacha mara mbili . Toka mwaka 1989 mpaka mwaka 2010.




   Mwaka 1989 Undertaker alimuoa mcheza mieleka mwenzake bibie Jodi Lynn,na  ndiye alikuwa mke wa kwanza walibahatika kupata mtoto mmoja. 




GUNNER VICENT CALAWAY
Gunner Vicent Calaway kazaliwa mwaka 1993.Ila ilipofika mwaka 1999 wawili hao walitengana(waliachana)
  Mwaka 21 july mwaka 2000 ndipo alipofunga ndoa na mke wake wapili Sara Calaway katika kanisa la St.Petersburg huko Frlida Inchini Marekani.
UNDERTAKE SIKU YA NDOA NA SARA CALAWAY

 Sara Calaway pia alikuwa ni mchezaji wa mieleka,


GRACIE CALAWAY MTOTO WA UNDERTAKER
MTOTO WA PILI WA UNDERTAKER
CHASEY CALAWAY MTOTO WAPILI WA UNDERTAKER

  Walibahatika kupata watoto wawili wa kike,Chasey Calaway kazaliwa (21 November 2002).na Gracie Calaway kazaliwa (15 may 2005).Hata hivyo naye hakudumu hatimaye ndoa yao ikavunjika  mwaka 2007.


MICHELLE MC COOL
   Akaja kuwa na mahusiano ya kimapenzi nakuungana na mchezaji wa mieleka wa zamani Michelle Mc cool 


UNDERTAKER AKIFUNGA NDOA NA MKE WAKE WA TATU MICHELLE MC COOL
na hatimaye wakafunga ndoa 26 june 2010 katika mji wa Houstin Texas huko nchini marekani.Hata hivyo 29 august 2012 wawili hao wakabahatika kupata mtoto wa kike,na kumpatia jina Kaia Faith Calaway.


KAIA FAITHY  MTOTO WA WANNE WA UNDERTAKER ALIYEBEBWA
Na hivyo kutimiza idadi ya watoto wanne wa Undertaker wakiume mmoja na wakike watatu.
Mwandishi wa Gazet la Telegraph Tom Fordy alimtaja  Undertaker kuwa ni the world’s greatest sportsman,Na vile vile mwaka  2015 Undertaker akawa mchezaji mieleka wa kwanza   Aliyesainiwa  na kudumu ndani ya WWE Chini  ya  Brand ya SMACK DOWN toka 1990 na kutanua taaluma ya kazi yake kwa miaka 25 ndani ya kampuni hiyo.



 Undertaker Ana kaka zake wanne David,Michael ,Paul,Timothy.
Undertake uzito wa kilo 140 na urefu wa futi 6.10 ambayo ni sawa na Mita 2.08. Majina ya Utani ya Undertaker ni ,Texas Red,The Punisher na Master of Pain .
Inakadiriwa kuwa Undertaker ana Utajiri wa Dola Milion 16.


Hakuna maoni: