Jumatatu, 14 Novemba 2016

AINA ZA WANYAMAPORI MAISHA NA TABIA ZAO


        UNDAMILIA-ZEBRA
     Mnyama huyu hutambulika kutokana na mistari yake ya pekee yenye mvuto ilipangilika vizuri nyenye weusi na weupe unaovutia.wanyama hawa wana patikana katika maeneo ya grassland,shrubland, milimani na grassland of Africa.Wanyama hawa chakula chao kikuu ni majani .

Pundamilia wakila majani

 hawezi kuishi kuishi bila ya kunywa maji .na huitajika kunywa angalau mara moja kwa siku.
Pundamilia wakinywa Maji

Wanasayansi wa masuala ya Viumbe wanaamini kuwa kutokana na utafiti wanyama (identification of animals) ya kuwa Pundamilia asili yake ni mnyama mwenye ngozi nyeusi ila tu kafuniko na mistari ya weupe.
   pundamilia ana urefu wa Futi 3.5 hadi 5 katika mabega na uzito wa kilo 200 mpaka 450 ambayo ni sawa na pound  440-990


Pundamillia katika kundi la swala

Wanyama hawa huishi kwenye kundi kubwa kwa zaidi ya wanyma 1000,na kuna wakati hujichangana na swala.
Kundi la familia ndogo ya Pundamilia
  Ndani ya kundi kubwa kuna familia ndogo ambayo hiyo huwa na dume mmoja,pamoja na majike wachache wa familia moja,
Simba akimkibiza pundamilia
dume na jike huakikisha wanatoa ulinzi wa kutosha juu ya watoto wao.Dume hujaribu kuwapeleka madui mbali inapotokea kesi ya mashambulizi.
Pundamilia wanakimbia katika kundi kubwa
   Mara tu wanapovamiwa hukimbia upande mmoja na mwingine katika mfumo wa zigzag hii ni katika hali ya kumchanganya adui.
   Pundamilia ni wanyama wanaokimbia  kasi kwa umbali wa mile 35 kwa saa ambayo ni sawa na kilometa karibu 70.Na pia mtoto wa pundamilia huweza kukimbia  saa moja tu baada ya kuzaliwa,

PUNDAMILIA DAKIKA MCHACHE BAADA YA KUZALIWA
 Wanyama hawa wanauwezo mzuri wa kuona na kusikia. Na zaidi ya hapo wanyama hawa hulala hali ya kuwa wamesimama.Pundamilia dume hujulikana kama Stallin na kwa upande wa jike hufahamika kama mare.

Dume la Pundamilia ni Stallion

Jike ni Mare
  
  Baadhi ya pundamilia huhama kipindi cha msimu wa ukame,huweza kusafiri kwa zaidi ya umbali wa mile 500 kwa kila mwaka kutafuta chakula na maji ya kutosha.  Na  zaidi ya hapo wanyama hawa hulala hali ya kuwa wamesimama.
   Pundamilia wanaishi kati ya umri wa miaka 20 na 30 porini na kwa mbukani huishi mpaka wa miaka 40.

      mtambue chui mweusi-(PANTHER )




    Ni aina ya jamii ya paka pori wakubwa ambao wanapatikana katika bara la America, Asia na Africa,Mnyama huyu hufanana sawa na chui asiye na madoa. wanyama hawa ngozi ya manyoya yao ni tofauti wapo wenye rangi ya manjano au hudhurungi (dark brown fur )na macho ya alimasi(yanaong’aa kama zumari)


Chui mweusi mwenye macho ya almasi

hujulikana kama black jaguar huko Latini America,na Black Leopard Katika bara la ASIA na Africa ila kwa upande wa amerika kaskazini(North America )Hufahamika
 kama Black Cougar.,wenye rangi ya manjano na panther weusi ni katika jamii moja ya wanyama hawa.



CHUI MWEUSI AKILA KICHWA CHA MNYAMA


Chui mweusi akila Nyama
Ni mnyama mla nyama (Carnivores),Licha ya wanyama wadogo bali pia ndege,jamii zote za nyoka na wanyama wakubwa.


Chui mweusi akimvuta nyoka
  makazi yake ni katika misitu mikubwa, pembezoni mwa mabawa(Swamps,)
savanna,milimani na hata jangwani.
  Chui huyu mweusi ana erefu wa fut 7 – 8 na uzito wa pound 100-250 ambayo ni sawa na kilo 45.45 mpaka 113.65.


Panther ni mnyama anayeishi kipweke (solitary)hukutana mara tu msimu wa kujamiana unapofika,baada ya miezio kadhaa ya ujauzito jike huzaa watoto wawili 2 mpaka 4.Ila kazi ya kulea watoto hufanywa na jike mwenyewe.




           watoto wa chui mweusi
-
Watoto hujifunza kupanda miti mwanzoni wadogo wao,ni wapandaji wa miti imara miongoni mwa jamii ya paka dunia.macho ya watoto mwanzoni wanapozaliwa huwa yamefumba na kufunikwa na manyoya  mepesi (light fur)






  Baada ya kufikisha umri wa miezi 2-hadi 3 watoto huanza kufundishwa kuwinda na mama yao.
Kiasi cha miezi 8 toka kuzaliwa mtoto panther kutokana na wepesi wa kujifunza na kuelewa kwa haraka kisha kuingia katika utendaji. basi huweza kuwinda na kukamata wanyama wa size ya kati. 


CHUI MWEUSI NI MWENYE KONO KUBWA
 Black panther ni mmnyama mwenye kono kubwa na imara lenye makucha makali kuliko aina zingine za jamii za paka na hilitumia kono lake hilo kubwa wakati akiwinda.Hunguruma kwa sauti kubwa na ya kutisha, mnyama huyu ana uwezo wa kuruka juu kwa umbali wa futi 20.


    Black panter anaweza kuishi na kuzoea kwa haraka katika eneo lenye makazi ya watu kuliko wanyama wengine wa jamii yake . mnyama huyu Ana uwezo mkubwa wa kuona na pia hisia kali za kusikia. 



Ni mwenye uwezo mkubwa wa kuona



PANTHER AKIPANDA MITI

Panther ni miongoni mwa wanyama walio hatarini kutoweka .kutokana na sababu mbali mbali kosefu wa makazi,uwindaji ulikithiri ,uhalibifu wa mazingira na ongezeko la joto duniani(global warming.)
   
Chui mweusi akiwa kakaa Porini

Chui wanaofungwa

  Chui mweusi huishi (Panther)umri wa miaka 12 Porini na kwa wale wanaofungwa huishi miaka 20.

























HUYU NI MNYAMA WA AJABU KUANZIA MUONEKANO HADI TABIA NA MWENEDO WAKE.

ANTEATER


giant anteater

Ni mnyama mwenye asili ya America ya kati na Kusini ,hasa katika inchi za Brazil,Bolivia na Argentina,alimkubwa kabisa ana urefu wa futi 5.11pamoja na mikia,na uzito wa kilo 39.ni mnyama mkubwa asiye na meno sawa na umbile la mbwa ama zaidi ya hapo,ni mwenye kichwa chembamba kirefu


ANTEATER AKITOA ULIMI.

na ulimi mrefu kiasi cah mita mbili,shingo ni pana kuliko kichwa ana manyoya mengi mkiani.
ANTEATER NA MKIAWENYE MANYOYA MENGI

,kama utamuangalia kwa wasiwasi unaweza dhani mbele ndio nyuma na nyuma ndio mbele,ukweli anashangaza


ANASHANGAZA KWA RANGI NA UMBO

Ana macho dhaifu yasio na uwezo mzuri wa kuona,ila ana sensor kali ya kunusa harafu mara40 zaidi ya mwandamu.


Mnyama huyu anamahusiano ya karibu na wanyama wa jamii yake kama Kakakuona(armadillo)sloth ,Aardivark na Pangolin.

KUNA SPECIE 4 ZA WANYAMA HAWA

(1)northern tamandua(tamandua Mexicana).


NORTHERN TAMANDUA

(2)sourthen tamandua (tamandua tetradactyla)


SOUTHERN TAMANDUA


(3)Sillky aneater(cyclopes didactylus

SILLKY ANTEATER

(4) Giant ant eater(myrmecophaga tridactyla

GIANT ANTEATER

makazi yake makuu ni msituni,ni mnyama anayelala mchana na kuamka usiku,mara chache utamkuta akitafuta chakula mchana,chakula chake kikubwa sana ni wadudu aina ya mchwa,na wadudu wengine kama dudu chungu,mara zote hutembelea sana vichuguu na magogo, amabyo ni makazi ya wadudu hao,kama shamba lake la chakula ,ni mwenye makucha marefu,huyatumia kuchana,ama kuchimba ila kupata tundu la kutosha kupitisha ulimi wake ,ili kuwanasa wadudu hao,zoezi hilo hufanyika kwa dakika moja tu,kitendo cha kutia ulimi ,mara wadudu wanaponasa ,hunyonganyonga ulimi wake mara 150 kwa dakika 1 na kuwatia mdomo,kuwapondaponda na kuwameza,kisha huham kwenda kichuguu kingine,kwa siku hutembelea makazi ya wadudu 200 na hula kiasi cha wadudu elfu thelathini 35,000 kwa siku.
hata hivyo ni wanyama wanaoshi single single,ni wanyama ambayo walionajisia moja hawawezi kukaa pamoja dume na dume,mara mmoja miongoni  mwao anapoingia makazi ya mwezake huzuka ugomvi mkubwa na kumtoa katika mmiliki ya eneo lake ,kila dume hutawala eneo la upana wa kilometa 2,ila hutokea kuwa pair jike na dume pale kinapofika kipindi cha kujamiana.Dume hujisogeza kwa jike.dume huonyesha ishara ya mbalimabli za kupenda ,kwa kumnusanusa jike mithili ya mbuzi beberu, na wakati mwingine humbembeleza kibabe,dume na jike watadumu kwa siku tatu mfululizo ,wakipanda kila wakati wawezavyo,

mara jike anaposhika ujauzito hudumu nao kwa siku  190.
hatimae hujifungua mtoto mmoja,mwenye kilo 1.4. huzaliwa hali kafumba macho  huanza kufungua na kuanza kuona baada ya siku 6. ila hutokea mara chache sana kujifungu mapacha.
ANTEATER AKIWA KAMBEBA MWANAYE MGONGONI

mtoto hunyonya na kisha hubebwa mgongoni wakati,atambeapo hali akitafuta chakula.huwasiliana na mwanaye kwa njia mluzi na kisah humbeleleza akitumia ulimi wakwe


,jike huendelea kumnyonyesha kwa miezi 9 mara anapofikisha 10 huanza maisha ya kujitemea mwenyewe na kaunza kula vyakula vingine.
Hupevuka na kuanza kujamiana anapofikisha miaka 2 hadi 4.
maadui wa kubwa sana ni chui na wanya wengine wala nyama.
huishi kwa umri wa miaka 16.
 

Hakuna maoni: